Mnamo Mei 23, 2013 Serikali ya Uswiss kupitia Shirika lake la Misaada kwa kifupi SDC lilisaini makubaliano na Jimbo Katoliki Ifakara wa uboreshaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Francis iliyopo Mjini Ifakara. Katika Mkataba huo, SDC itafanya upanuzi wa baadhi ya maeneo ya huduma kama vile chumba kikuu cha upasuaji, kujenga chumba cha upasuaji kwa akina mama wanaojifungua, kujenga jengo jipya la utawala na ofisi za waganga, kujenga ukumbi mpya wa mikutano nk. Mkataba huo unahusu pia uboreshaji wa utoaji huduma na uongozi ambapo SDC kupitia Shirika la VSO - Volunteer Service Oversees limetoa wataalamu watatu katika nyanja za Utawala na Uongozi, Utabibu na Fedha ilikusaidia kuboresha maeneo hayo. Mkataba huu ambao utadumu kwa miaka mitatu, ulisainiwa na Askofu wa Jimbo Katolii Ifakara Mhashamu Salutaris Libena kwa niaba ya Jimbo la Ifakara na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Bwana Olivier Chave kwa niaba ya Serikali ya Uswisi. Walioshuhudia kusainiwa kwa mkataba huo kwa upande wa J...