Padri Louis Adalbert Mdenkeri alikuwa mtoto wa tatu kati ya watoto wanane kwa baba Adalbert Fidelis Mdenkeri na mama Anthonia Kazingoma. Alizaliwa Kwiro tarehe 31 Machi, 1945. Alibatizwa tarehe 01 Aprili, 1945 namba yake ya ubatizo: Kwiro LB 15093. Alipewa kipaimara na Hayati Askofu Mkuu Edgar Maranta tarehe 01 Oktoba, 1955 namba yake ikiwa LN 10026. Alipewa daraja ya Upadri huko Kwiro tarehe 12 Agosti, 1972 na hayati Askofu Adrian Mkoba wa Morogoro. MAREHEMU PADRE LOUIS MDENKERI Elimu: Hayati Padri Mdenkeli alisoma darasa la i-iv katika shule ya Msingi Kwiro. Baadaye seminari ndogo ya Mt. Fransis sasa inafahamika zaidi kama Kasita Seminari darasa la tano hadi la kumi. Baada ya kumaliza darasa la kumi pale Kasita aliacha seminari na kujiunga na sekondari ya Mt. Joseph – Jimbo Kuu la Dar es Salaam ambayo baadaye ikaja kuitwa Forodhani secondary school. Wakati anasoma St. Joseph sekondari, Hayati Sr. Yasinta aliyekuwa Mkuu wa shule alimshauri wakati huo k...