KONGAMANO LA UTOTO MTAKATIFU KANDA YA MASHARIKI 13 – 17/6/2013 JIMBONI IFAKARA Jimbo Katoliki Ifakara lilikuwa mwenyeji wa Kongamano la mwaka huu la Utoto Mtakatifu Kanda ya Mashariki ya Metropolitan ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Kongamano hilo lilifanyika kati ya tarehe 13 na 17 Juni, 2013 lilihusisha majimbo manane ambayo ni Ifakara, Mahenge, Morogoro, Dodoma, Kondoa, Tanga, Zanzibar na Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Jumla ya Watoto 2 512 na walezi 570 walishiriki kongamano hili. Jumla hii ya walezi inajumuisha pia Mapadri na Watawa Masista. Maaskofu walioshiriki walikuwa ni pamoja na Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Wahashamu Maaskofu Telesphore Mkude wa Morogoro, Agapit Ndorobo wa Mahenge, Eusebius Nzigirwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Askofu Mwenyeji Salutaris Libena. Jimbo mwenyeji liliwakilishwa na jumla ya watoto 875na walezi 89. Watoto na Walezi kutoka ndani ya Jimbo waliwasili Jimboni tarehe 10 Ju...
Comments
Post a Comment