- SIKU YA MWANAMKE DUNIANI WAWATA WAKUTANA MPANGA
Tarehe 8
Machi ya kila mwaka huadhimishwa kama Siku ya Mwanamke Duniani. Kijimbo,
Wanawake wakatoliki maarufu WAWATA waliiadhimisha siku ya Mwanamke Duniani ngazi
ya Jimbo katika Tarafa ya Mlimba Parokiani Mpanga. Ilikuwa siku nzuri pale
akina mama kutoka parokia mbalimbali walipokutana kwa semina, mafunzo
mbalimbali na siku ya kilele Misa Takatifu na michezo. Mgeni rasmi katika
kilele hicho alikuwa Mhe. Pd. Bonaventure Mchalange Naibu wa Askofu wa Ifakara.
Mahudhurio ya akina mama kadili ya parokia yalikuwa kama inavyoonekana kwenye
jedwali.
Na
|
Parokia
|
Idadi
|
Mwendelezo
|
|||
1
|
Taweta
|
16
|
11
|
Ifakara
|
29
|
|
2
|
Mpanga
|
47
|
12
|
Kibaoni
|
10
|
|
3
|
Mlimba
|
24
|
13
|
Kiberege
|
2
|
|
4
|
Chita
|
12
|
14
|
Mkula
|
11
|
|
5
|
Merera
|
11
|
15
|
Msolwa Ujamaa
|
1
|
|
6
|
Mchombe
|
21
|
16
|
Nyandeo
|
14
|
|
7
|
Mbingu
|
26
|
17
|
Mofu
|
0
|
|
8
|
Namwawala
|
3
|
18
|
Lungongole
|
0
|
|
9
|
Idete
|
3
|
19
|
Kisawasawa
|
0
|
|
10
|
Mahutanga
|
2
|
20
|
Mang’ula
|
0
|
|
…….
|
……………………..
|
……………
|
21
|
Kilombero
|
0
|
|
…….
|
………………………
|
…………….
|
……..
|
Jumla kuu
|
232
|
Katika picha matukio ya siku ya
kilele cha siku ya mwanamke kijimbo.
- SR HILTRUDA LYANIHELA ATUTOKA GHAFLA
Ilikuwa taarifa ya ghafla na ya kusikitisha sana pale Mama Mkuu wa Shirika la Masistaa wa Upendo wa Mt. Fransis wa Assis Jimbo la Mahenge alipotutangazia kifo cha Sr. Hiltruda. Sr. Hiltruda alifariki kwa ajali ya kugongwa na pikipiki maarufu “Bodaboda” asubuhi ya jumapili ya tarehe 14 Juni, 2015 eneo la Msimbazi Centre – Dar es Salaam alipokuwa akivuka barabara ya Kawawawa akielekea kanisani kwa misa ya dominika. Msamaria mwema alimwokota Sr. Hiltruda akiwa mahututi na kumkimbiza katika hospitali ya amana – Ilala na baada ya Uongozi wa Shirika kupata taarifa ulikwenda hospitalini na kumhamishia katika hospitali
ya Taifa Muhimbili. Pamoja na juhudi za madtari kuokoa uhai wake, Sr. Hiltruda alifariki dunia majira ya saa 5 asubui. Sr. Hiltruda alizikwa katika makaburi ya Masista Itete tarehe 17 Juni, 2015. Sr. Maria Hiltruda alizaliwa mwaka 1942 Kwiro Mahenge kwa baba Paulo Chigumbi Lyanihela na mama Maria Kamando, amefariki akiwa na umri wa miaka 73. Sr. Hiltruda alitegemewa kuadhimisha jubilei ya miaka 50 ya utawa mwakani, 2016.
APUMZIKE KWA
AMANI
- KWA HERI PADRI DISMAS UBISHIMBALI “STABLE”
Mtu wa watu, mtani,
mcheshi, muwazi, asiye na kinyongo Pd. Dismas Ubishimbali alitoweka ghafla kama
utani vile. Ilikuwa asubuhi ya tarehe 30 Mei, 2015 pale Mapadri na Watumishi wa
Nyumba ya Mapadri Ifakara walipoingia chumbani mwake alimofikia na kumkuta
akiwa amefariki. Pd. Ubishimbali alikuwa amefika Ifakara akitokea Kwiro kwa
lengo la kuhudhuria mazishi ya Baba Mdogo wa Padri Filbert Mhasi. Pd.
Ubishimbali ambaye alijiita na kutambulika kwa majimba ya utani kama vile
“mzungu”, “mzungu mpakistani”, “stable”, nk. Alizaliwa 15/02/1950 kwa baba
Clarence Michael Ubishimbali na mama Clara Iddi Antoni Ubaratu. Kwa asili Pd.
Ubishimbali ni mzaliwa katika kijiji cha Ebuyu wakati huo ikiwa chini ya Parokia
ya Sali Jimbo la Mahenge na familia yake ilihamia Ifakara miaka ya 1964/65. Alisoma
Kasita na baadaye Seminari Kuu ya Ntungamo na kumalizia Kipalapala Tabora.
Alipata daraja ya ushemasi 29/06/1975 na upadrisho 14/08/1976, madaraja yote
aliyapata kwa Askofu Patrick Iteka. Alifariki usiku wa kuamkia 30/05/2015 na
kuzikwa Kwiro 02/06/2015.
APUMZIKE KWA AMANI
- SFUCHAS WAOMBOLEZA
Jumuiya ya
Chuo Kikuu kishiriki cha Tiba cha Chuo Kikuu cha Mt. Augustino cha Tanzania tawi
la Ifakara ilipatwa na msiba mkubwa wa kufiwa na mmoja wa wanafunzi wa chuo
hicho kijana Samweli Lucas. Kijana Samweli alifariki katika ajali ya barabarani
katika Mbuga ya Mikumi tarehe 19 Machi, 2015 baada ya basi alilokuwa akisafilia
kuja/kurudi Ifakara baada ya likizo fupi ya wiki mbili kugongana uso kwa uso na
lori la mizigo na yeye kufariki hapohapo. Marehemu Sanweli alikuwa mwanafunzi
wa mwaka wa kwanza wa kozi ya uganga/udaktari. Kichuo alikuwa Waziri wa Ulinzi
katika Serikali ya Wanafunzi ya chuo na mwanamichezo mzuri. Hayati Samweli aliagwa
rasmi na jumuiya wa Chuo na wakati wa Ifakara 23/03/2015 na alikizikwa nyumbani
kwao Kibaha 24/03/2015.
APUMZIKE KWA
AMANI
Picha ya Marehemu Samweli wakati wa uhai wake Baba Askofu wa Ifakara na
waombolezaji wengine wakitoa heshima zao za mwisho
- HOSTELI KIKWAWILA
Mapadri wa
Shirika la Utangazaji wa Habari Njema (Heralds of Good News) wanaosimamia kituo
cha Watoto Yatima na Wazee cha Kikwawila wamefungua hosteli yao ya wageni
iliyokuwa katika ujenzi kwa miaka mingi. Ujenzi wa hosteli hii ulianza na Pd.
Fransis aliyekuwa mwanzilishi wa kituo hicho. Pamoja na nguvu za Shirika, ujenzi wa hosteli
hii umepata pia msaada kutoka kwa Wanashirika la “Association Gocce” wa Italia
na Mama Maria Tan wa Singapore. Hosteli hii ilibarikiwa na kufunguliwa na
Mhashamu Salutaris Libena Askofu wa Ifakara tarehe 16/05/2015 na tukio hilo
kushuhudiwa na wawakilishi wa “Association Gocce” ambao ni Anna, Fabian na
Torante anayefanyakazi Chuo cha Manesi cha Edgar Maranta.
- ASHEREHEKEA MIAKA 20 YA UASKOFU
Mhashamu Agapiti Ndorobo Askofu
wa Jimbo la Mahenge aliadhimisha Jubilei Ndogo ya kutimiza Miaka 20 ya Utumishi
katika Jimbo la Mahenge kama Askofu. Sherehe hii ilifanyika tarehe 16/06/2015
kwa misa takatifu iliyoanza kuanzia saa 10 jioni katika Kanisa Kuu la Kristo
Mfalme Kwiro na baadaye kufuatiwa na tafrija kubwa na nzuri. Askofu Ndorobo
alitangazwa kuwa Askofu wa Mahenge 21/03/1995 na kusimikwa rasmi 16/06/1996.
Sisi Wanajimbo la Ifakara tunampongeza sana Baba Askofu kwa kutimiza miaka hii
ya utumishi kama Askofu na tunamwombea Baraka za Mwenyezi Mungu apate afya njema
na nguvu zaidi za kulitumikia taifa la Mungu.
What is the best gambling site? (2021)
ReplyDeleteCasino 군산 출장샵 Sites have the ability to offer some 군포 출장샵 kind of casino services. You can 구리 출장마사지 browse the 태백 출장마사지 list of games and choose 안전 토토 사이트 which ones you want to play.