MSHUMAA MKUBWA WA MWAKA WA IMANI Mnamo tarehe ya 17 ya mwezi wa 11 mwaka 2012, Mhashamu Askofu Salutaris M. Libena wa Jimbo Katoliki la Ifakara alizindua rasmi MWAKA WA IMANI katika Kanisa Kuu la Jimbo la Mtakatifu Andrea - Ifakara. Katika Misa hiyo Mhashamu Baba Askofu aliwasha Mshumaa Mkubwa wa Mwaka wa Imani na kisha kuwasha mishumaa midogo kutoka Mshumaa Mkubwa na kuwakabidhi Maparoko kwenda nayo Maparokiani kwo. Na ujumbe "MKAMTANGAZE KRISTO KWA KILA KIUMBE". Miongoni mwa maazimio ya Mwaka wa Imani Jimboni Ifakara ni kuutembeza MSALABA katika Parokia zote ndani ya Jimbo. Mbio hizo za kuutembeza Msalaba zimeanza leo tarehe 29/12/2012 kutokea Kanisa kuu la Jimbo na kwenda kukabidhiwa Parokia ya TAWETA ambayo inapakana na Jimbo la Njombe. Msalaba huo umeenda kukabidhiwa na Mhashamu Askofu Salutaris M. Libena. Ratiba ya mzunguko wa Msalaba huo imetoka, Safari ya Msalaba itakuwa kam...