Leo tarehe 26/12/2012 Madhehebu ya Kikristo Mjini Ifakara yamefanya Tamasha la Kwaya za Kikristo kama sehemu mojawapo ya Uinjilishaji. Maaskofu wawili walishiriki Tamasha hilo, ambao ni Mhashamu Askofu Salutaris M. Libena wa JImbo Katoliki la Ifakara na Askofu Lenard Mtenji wa KKKT Usharika wa Ifakara.
Mhashamu Askofu Salutaris Libena wa Jimbo Katoliki la Ifakara aliwaambia Wanakwaya wa Kwaya zote kuwa Utume wao si kuimba kama wengine wanavyofikiri, bali UTUME WAO NI UINJILISHAJI KWA NJIA YA KUIMBA. Kwa hiyo aliwaambia wanapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwajalia sauti nzuri za kuimba, kwa hiyo wazitumie sauti hizo KUMSIFU, KUMUABUDU, KUMTUKUZA, KUMSHUKURU NA KUMTANGAZA MWENYEZI MUNGU KWA WATU WOTE.
Pia aliwaomba watunzi wa nyimbo watunge nyimbo za Kumsifu, Kumtukuza na Kumshukuru Mwenyezi Mungu na Yesu Kristo zaidi kuliko kutunga nyimbo zinazomtaja SHETANI MWANZO MWISHO.Kwani tumepewa silaha za kujikinga na huyo shetani, lakini licha ya kupewa hizo kinga tumepewa silaha ya kupambana naye. Hiyo ni PANGA ambalo ni NENO LA MUNGU ambalo linakata kuwili. Kwa hiyo tutumie Neno la Mungu ambalo shetani hapendi kulisikia mara kwa mara. Kwa maana hiyo TULIIMBE, TULISOME NA TULIUBIRI NENO LA MUNGU WAKATI WOTE.
Katika Tamasha hilo wanakwaya wa kwaya mbalimbali waliinjilisha kwa kina kwa kupitia mtindo wa kuimba.Baadhi ya Madhehebu ya Kikristo ambayo yalishiriki Tamasha hilo ni WAKATOLIKI, WALUTHERI, WAANGLIKANI, WABAPTIST NA MOROVIANI.
Washiriki wameonesha kuridhika na maandalizi yalivyofanywa. Tendo hili limeonesha umoja wa Kanisa la Kristo. Madhehebu hayo yote yanamtangaza Kristo yule yule Mwana pekee wa Mungu, nafsi ya pili ya Mungu, Mungu halisi sawa na Mungu Baba.
Comments
Post a Comment