SIKU YA MWANAMKE DUNIANI WAWATA WAKUTANA MPANGA Tarehe 8 Machi ya kila mwaka huadhimishwa kama Siku ya Mwanamke Duniani. Kijimbo, Wanawake wakatoliki maarufu WAWATA waliiadhimisha siku ya Mwanamke Duniani ngazi ya Jimbo katika Tarafa ya Mlimba Parokiani Mpanga. Ilikuwa siku nzuri pale akina mama kutoka parokia mbalimbali walipokutana kwa semina, mafunzo mbalimbali na siku ya kilele Misa Takatifu na michezo. Mgeni rasmi katika kilele hicho alikuwa Mhe. Pd. Bonaventure Mchalange Naibu wa Askofu wa Ifakara. Mahudhurio ya akina mama kadili ya parokia yalikuwa kama inavyoonekana kwenye jedwali. Na Parokia Idadi Mwendelezo 1 Taweta 16 11 Ifakara 29 2 Mpanga 47 12 Kibaoni 10 3 Mlimba 24 13 Kiberege 2 4 Chita 12 14 Mkula 11 5 Merera 11 15 Msolwa Ujamaa 1 6 Mchombe 21 16
Padri Louis Adalbert Mdenkeri alikuwa mtoto wa tatu kati ya watoto wanane kwa baba Adalbert Fidelis Mdenkeri na mama Anthonia Kazingoma. Alizaliwa Kwiro tarehe 31 Machi, 1945. Alibatizwa tarehe 01 Aprili, 1945 namba yake ya ubatizo: Kwiro LB 15093. Alipewa kipaimara na Hayati Askofu Mkuu Edgar Maranta tarehe 01 Oktoba, 1955 namba yake ikiwa LN 10026. Alipewa daraja ya Upadri huko Kwiro tarehe 12 Agosti, 1972 na hayati Askofu Adrian Mkoba wa Morogoro. MAREHEMU PADRE LOUIS MDENKERI Elimu: Hayati Padri Mdenkeli alisoma darasa la i-iv katika shule ya Msingi Kwiro. Baadaye seminari ndogo ya Mt. Fransis sasa inafahamika zaidi kama Kasita Seminari darasa la tano hadi la kumi. Baada ya kumaliza darasa la kumi pale Kasita aliacha seminari na kujiunga na sekondari ya Mt. Joseph – Jimbo Kuu la Dar es Salaam ambayo baadaye ikaja kuitwa Forodhani secondary school. Wakati anasoma St. Joseph sekondari, Hayati Sr. Yasinta aliyekuwa Mkuu wa shule alimshauri wakati huo kijana Louis Mk