Skip to main content

Posts

KONGAMANO LA UTOTO MTAKATIFU WA YESU 2013

WATOTO WA UTOTO MTAKATIFU WA YESU Kongamano la Utoto Mtakatifu wa Yesu Kanda ya Mashariki 2013 litafanyika Jimboni Ifakara kuanzia tarehe 13 - 17 ya mwezi wa sita (6). Ni majimbo nane (8) yanayotarajiwa kushiriki katika Kongamano hilo. Majimbo hayo ni:- Dar es Salaam, Morogoro, Mahenge, Tanga, Zanzibar, Dodoma, Kondoa na Ifakara. Maandalizi ya Kongamano hilo yanaendelea vizuri. Mhashamu Askofu Salutaris Libena, Mapadre, Watawa na Waamini wote wa Jimbo la Ifakara wanawakaribisha Watoto wote na watu wote wenye mapenzi mema kufurahia ukarimu wa watu wa Jimbo la Ifakara..                                                     "MTOTO NA IMANI"                               KWA PAMOJA TUNASEMA KARIBUNI SANAA!! ...

MWAKA MMOJA WA JIMBO

Mnamo tarehe 19/03/2012 Jimbo Katoliki la Ifakara lilizinduliwa rasmi, na Mhashamu Askofu Salutaris Libena alisimikwa rasmi kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo la Ifakara. Leo 19/03/2013 Jimbo la Ifakara linatimiza Mwaka Mmoja tangu kuzaliwa rasmi. Jimbo katika kuonesha shukrani kwa Mungu limeadhimisha sherehe ya Mt. Yosefu Mume wa Bikira Maria. Katika adhimisho hilo la Misa Takatifu Mhashamu Askofu Salutaris Libena alisisitiza juu ya kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufanikiwa katika mambo mengi tuliyojipangia. Pia alisisitiza tuwe na Imani dhabiti kwa Mungu hasa katika Mwaka huu wa Imani. Imani hii juu ya Kristo iwe endelevu ili tuweze kufanikiwa katika mipango yetu. Misa hiyo ilihudhuriwa na Mapadre, Watawa na Walei. IFAKARA DIOCESE VIVA!

KWA HERI KATEKISTA NYONI

Parokia ya Ifakara inasikitika kumpoteza Katekista hodari Pius Pius Nyoni, ambaye Mwenyezi Mungu amependa kumuita kwake. Katekista Nyoni alizaliwa mwaka 1954 huko kijiji cha Sofi. Alipata elimu ya sekondari huko Mahenge Kwiro. Katekista  Nyoni alifanya kazi sehemu mbalimbali kabla ya kuanza kazi ya ukatekista. Alianza kazi ya Ukatekista mwaka 2003 hapa parokiani Ifakara akiwa kama mwezeshaji wa semina mbalimbali hasa katika kundi la wana uamsho. Alipelekwa chuo cha Makatekista na kisha kurudi parokiani na kuwa mwalimu wa dini mzuri. Waliofundishwa naye ndio mashaidi hasa wa utaalamu wa fani yake hii ya mwisho, yaani UALIMU WA DINI. Wote tunaalikwa kumuombea huyu ndugu yetu ambaye alifanya kazi ya Kuwafundisha watu juu ya Mungu na kuwapeleka kwa Mungu kwa mafundisho mbalimbali. APUMZIKE KWA AMANI.

MBIO ZA MWAKA WA IMANI ZA PAMBAMOTO - IFAKARA

MSHUMAA MKUBWA WA MWAKA WA IMANI       Mnamo tarehe ya 17 ya mwezi wa 11 mwaka 2012, Mhashamu Askofu Salutaris M. Libena wa Jimbo Katoliki la Ifakara alizindua rasmi MWAKA WA IMANI katika Kanisa Kuu la Jimbo la Mtakatifu Andrea - Ifakara. Katika Misa hiyo Mhashamu Baba Askofu aliwasha Mshumaa Mkubwa wa Mwaka wa Imani na kisha kuwasha mishumaa midogo kutoka Mshumaa Mkubwa na kuwakabidhi Maparoko kwenda nayo Maparokiani kwo. Na ujumbe "MKAMTANGAZE KRISTO KWA KILA KIUMBE".      Miongoni mwa maazimio ya Mwaka wa Imani Jimboni Ifakara  ni kuutembeza MSALABA katika Parokia zote ndani ya Jimbo. Mbio hizo za kuutembeza Msalaba zimeanza leo tarehe 29/12/2012 kutokea Kanisa kuu la Jimbo na kwenda kukabidhiwa Parokia ya TAWETA ambayo inapakana na Jimbo la Njombe. Msalaba huo umeenda kukabidhiwa na Mhashamu Askofu Salutaris M. Libena.      Ratiba ya mzunguko  wa Msalaba huo imetoka, Safari ya Msalaba itakuwa kam...

TAMASHA LA SHIRIKISHO LA KWAYA ZA KIKRISTO - IFAKARA

Leo tarehe 26/12/2012 Madhehebu ya Kikristo Mjini Ifakara yamefanya Tamasha la Kwaya za Kikristo kama sehemu mojawapo ya Uinjilishaji. Maaskofu wawili walishiriki Tamasha hilo, ambao ni Mhashamu Askofu Salutaris M. Libena wa JImbo Katoliki la Ifakara na Askofu Lenard Mtenji wa KKKT Usharika wa Ifakara. Mhashamu Askofu Salutaris Libena wa Jimbo Katoliki la Ifakara aliwaambia Wanakwaya wa Kwaya zote kuwa Utume wao si kuimba kama wengine wanavyofikiri, bali UTUME WAO NI UINJILISHAJI KWA NJIA YA KUIMBA. Kwa hiyo aliwaambia wanapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwajalia sauti nzuri za kuimba, kwa hiyo wazitumie sauti hizo KUMSIFU, KUMUABUDU, KUMTUKUZA, KUMSHUKURU NA KUMTANGAZA MWENYEZI MUNGU KWA WATU WOTE. Pia aliwaomba watunzi wa nyimbo watunge nyimbo za Kumsifu, Kumtukuza na Kumshukuru Mwenyezi Mungu na Yesu Kristo zaidi kuliko kutunga nyimbo zinazomtaja SHETANI MWANZO MWISHO.Kwani tumepewa silaha za kujikinga na huyo shetani, lakini licha ya kupewa hizo kinga tumepewa sil...

MWAKA WA IMANI 2012 - 2013

     Idara ya mawasiliano (J) Katoliki la Ifakara, inapenda kuwatangazia Mapadre, Watawa, Walei na watu  wenye mapenzi mema wa Jimbo la Ifakara na Kanisa kwa ujumla kuwa tarehe 17 /11 /2012 Mhashamu Baba Askofu Salutaris M. Libena atazindua rasmi MWAKA WA IMANI JIMBONI IFAKARA 2012 - 2013

THE SYNOD ON NEW EVANGELIZATION

AMECEA: Remembering the Synod on New Evangelization The Thirteen Ordinary General Assembly for the New Evangelization, which begun on 8 th October, ended on 28 th October with Holy Mass by the Holy Father, Pope Benedict XVI. The Holy Father offered a reflection on the Gospel reading of the day (John 9:39-41), which spoke about the healing of Bartimaeus, the last miracle Jesus performed before his passion.    The theme of the homily by the Holy Father was: “The New Evangelization Applies to the whole of the Church’s Life”. He stressed that the healing of Bartimaeus “represents man who needs God’s light, the light of faith, if he is to know reality truly and to walk the path of life. It is essential to acknowledge one’s blindness, one’s need for this light, otherwise one could remain blind forever. Bartimaeus represents man who has lost the light and knows it, but has not lost hope: he knows how to seize the opportunity to encounter Jesus and he entrusts himself to ...