Skip to main content

Posts

Showing posts from January 6, 2013

KWA HERI KATEKISTA NYONI

Parokia ya Ifakara inasikitika kumpoteza Katekista hodari Pius Pius Nyoni, ambaye Mwenyezi Mungu amependa kumuita kwake. Katekista Nyoni alizaliwa mwaka 1954 huko kijiji cha Sofi. Alipata elimu ya sekondari huko Mahenge Kwiro. Katekista  Nyoni alifanya kazi sehemu mbalimbali kabla ya kuanza kazi ya ukatekista. Alianza kazi ya Ukatekista mwaka 2003 hapa parokiani Ifakara akiwa kama mwezeshaji wa semina mbalimbali hasa katika kundi la wana uamsho. Alipelekwa chuo cha Makatekista na kisha kurudi parokiani na kuwa mwalimu wa dini mzuri. Waliofundishwa naye ndio mashaidi hasa wa utaalamu wa fani yake hii ya mwisho, yaani UALIMU WA DINI. Wote tunaalikwa kumuombea huyu ndugu yetu ambaye alifanya kazi ya Kuwafundisha watu juu ya Mungu na kuwapeleka kwa Mungu kwa mafundisho mbalimbali. APUMZIKE KWA AMANI.