Skip to main content

Posts

Showing posts from 2013

PADRE LOUIS MDENKERI HATUPO NAE TENA

Padri Louis Adalbert Mdenkeri alikuwa mtoto wa tatu kati ya watoto wanane kwa baba Adalbert Fidelis Mdenkeri na mama Anthonia Kazingoma. Alizaliwa Kwiro tarehe 31 Machi, 1945. Alibatizwa tarehe 01 Aprili, 1945 namba yake ya ubatizo: Kwiro LB 15093. Alipewa kipaimara na Hayati Askofu Mkuu Edgar Maranta tarehe 01 Oktoba, 1955 namba yake ikiwa LN 10026. Alipewa daraja ya Upadri huko Kwiro tarehe 12 Agosti, 1972 na hayati Askofu Adrian Mkoba wa Morogoro.   MAREHEMU PADRE LOUIS  MDENKERI   Elimu: Hayati Padri Mdenkeli alisoma darasa la i-iv katika shule ya Msingi Kwiro. Baadaye seminari ndogo ya Mt. Fransis sasa inafahamika zaidi kama Kasita Seminari darasa la tano hadi la kumi. Baada ya kumaliza darasa la kumi pale Kasita aliacha seminari na kujiunga na sekondari ya Mt. Joseph – Jimbo Kuu la Dar es Salaam ambayo baadaye ikaja kuitwa Forodhani secondary school. Wakati anasoma St. Joseph sekondari, Hayati Sr. Yasinta aliyekuwa Mkuu wa shule alimshauri wakati huo kijana Louis Mk

WATOTO WA KITUO CHA BETHLEHEM WAPATA AJALI

Watoto wapatao 103, Walezi na Wafanyakazi wa Kituo cha Bethlehem jumla yao yapata kama 160 walipata ajali ya gari siku ya jumanne ya tarehe 25 juni, 2013 majira ya saa 11 jioni wakati wakituri kutoka pikiniki. Ajali hiyo ilitokea eneo la Kijiji cha Kilama B baada ya Fuso lililo wabeba kuingia katika shimo na kuanguka. Kati ya Walezi waliopata ajali alikuwepo pia Sr. Salome. Masista wengine walezi walirudi kwa gai nyingine. Mkurugenzi wa Kituo cha Bethlehem, Padri Basil Ngwega alieleza kuwa Watoto, Walezi na Wafanyakazi wa Kituo cha Bethlehem huwa na kawaida ya kufanya pikiniki wakati wanapofunga likizo la mwaka. Na mara hii walichagua kwenda Kilama B kwa pikiniki. Aliendelea kusema kuwa wakati wakirudi, gari ambalo lilibeba kundi kubwa zaidi lilitumbukia kwenye mtaro na kuegama baadaye kuanguka upande wa kulia mwa gari. Katika ajali hiyo, watoto wapatao 20 na walezi 5 waliweza kupata majeraha mbalimbali. Kati yao watoto 2 waliumia kichwani na kushonwa na walezi 4 walipumzishwa kati

KONGAMANO JIMBONI IFAKARA

KONGAMANO LA UTOTO MTAKATIFU KANDA YA MASHARIKI 13 – 17/6/2013 JIMBONI IFAKARA  Jimbo Katoliki Ifakara lilikuwa mwenyeji wa Kongamano la mwaka huu la Utoto Mtakatifu Kanda ya Mashariki ya Metropolitan ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Kongamano hilo lilifanyika kati ya tarehe 13 na 17 Juni, 2013 lilihusisha majimbo manane ambayo ni Ifakara, Mahenge, Morogoro, Dodoma, Kondoa, Tanga, Zanzibar na Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Jumla ya Watoto 2 512 na walezi 570 walishiriki kongamano hili. Jumla hii ya walezi inajumuisha pia Mapadri na Watawa Masista. Maaskofu walioshiriki walikuwa ni pamoja na Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Wahashamu Maaskofu Telesphore Mkude wa Morogoro, Agapit Ndorobo wa Mahenge, Eusebius Nzigirwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Askofu Mwenyeji Salutaris Libena. Jimbo mwenyeji liliwakilishwa na jumla ya watoto 875na walezi 89. Watoto na Walezi kutoka ndani ya Jimbo waliwasili Jimboni tarehe 10 Juni s

MATUKIO YA KUSAINIWA MKATABA WA MSAADA KATI YA JIMBO LA IFAKARA NA SERIKALI YA USWISI

ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI LA IFAKARA  SALUTARIS M. LIBENA NA BALOZI  WA USWIZ  WAKIBADILISHANA MKATABA     WAKIPONGEZANA BAADA YA KUSAINI MKATABA         PICHA YA PAMOJA BAADA YA KUSAINI MKATABA NDANI YA MAKAZI YA  ASKOFU  WA JIMBO LA IFAKARA                                       
Mnamo Mei 23, 2013 Serikali ya Uswiss kupitia Shirika lake la Misaada kwa kifupi SDC lilisaini makubaliano na Jimbo Katoliki Ifakara wa uboreshaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Francis iliyopo Mjini Ifakara. Katika Mkataba huo, SDC itafanya upanuzi wa baadhi ya maeneo ya huduma kama vile chumba kikuu cha upasuaji, kujenga chumba cha upasuaji kwa akina mama wanaojifungua, kujenga jengo jipya la utawala na ofisi za waganga, kujenga ukumbi mpya wa mikutano nk. Mkataba huo unahusu pia uboreshaji wa utoaji huduma na uongozi ambapo SDC kupitia Shirika la VSO - Volunteer Service Oversees limetoa wataalamu watatu katika nyanja za Utawala na Uongozi, Utabibu na Fedha ilikusaidia kuboresha maeneo hayo. Mkataba huu ambao utadumu kwa miaka mitatu, ulisainiwa na Askofu wa Jimbo Katolii Ifakara Mhashamu Salutaris Libena kwa niaba ya Jimbo la Ifakara na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Bwana Olivier Chave kwa niaba ya Serikali ya Uswisi. Walioshuhudia kusainiwa kwa mkataba huo kwa upande wa J

KONGAMANO LA UTOTO MTAKATIFU WA YESU 2013

WATOTO WA UTOTO MTAKATIFU WA YESU Kongamano la Utoto Mtakatifu wa Yesu Kanda ya Mashariki 2013 litafanyika Jimboni Ifakara kuanzia tarehe 13 - 17 ya mwezi wa sita (6). Ni majimbo nane (8) yanayotarajiwa kushiriki katika Kongamano hilo. Majimbo hayo ni:- Dar es Salaam, Morogoro, Mahenge, Tanga, Zanzibar, Dodoma, Kondoa na Ifakara. Maandalizi ya Kongamano hilo yanaendelea vizuri. Mhashamu Askofu Salutaris Libena, Mapadre, Watawa na Waamini wote wa Jimbo la Ifakara wanawakaribisha Watoto wote na watu wote wenye mapenzi mema kufurahia ukarimu wa watu wa Jimbo la Ifakara..                                                     "MTOTO NA IMANI"                               KWA PAMOJA TUNASEMA KARIBUNI SANAA!!  

MWAKA MMOJA WA JIMBO

Mnamo tarehe 19/03/2012 Jimbo Katoliki la Ifakara lilizinduliwa rasmi, na Mhashamu Askofu Salutaris Libena alisimikwa rasmi kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo la Ifakara. Leo 19/03/2013 Jimbo la Ifakara linatimiza Mwaka Mmoja tangu kuzaliwa rasmi. Jimbo katika kuonesha shukrani kwa Mungu limeadhimisha sherehe ya Mt. Yosefu Mume wa Bikira Maria. Katika adhimisho hilo la Misa Takatifu Mhashamu Askofu Salutaris Libena alisisitiza juu ya kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufanikiwa katika mambo mengi tuliyojipangia. Pia alisisitiza tuwe na Imani dhabiti kwa Mungu hasa katika Mwaka huu wa Imani. Imani hii juu ya Kristo iwe endelevu ili tuweze kufanikiwa katika mipango yetu. Misa hiyo ilihudhuriwa na Mapadre, Watawa na Walei. IFAKARA DIOCESE VIVA!

KWA HERI KATEKISTA NYONI

Parokia ya Ifakara inasikitika kumpoteza Katekista hodari Pius Pius Nyoni, ambaye Mwenyezi Mungu amependa kumuita kwake. Katekista Nyoni alizaliwa mwaka 1954 huko kijiji cha Sofi. Alipata elimu ya sekondari huko Mahenge Kwiro. Katekista  Nyoni alifanya kazi sehemu mbalimbali kabla ya kuanza kazi ya ukatekista. Alianza kazi ya Ukatekista mwaka 2003 hapa parokiani Ifakara akiwa kama mwezeshaji wa semina mbalimbali hasa katika kundi la wana uamsho. Alipelekwa chuo cha Makatekista na kisha kurudi parokiani na kuwa mwalimu wa dini mzuri. Waliofundishwa naye ndio mashaidi hasa wa utaalamu wa fani yake hii ya mwisho, yaani UALIMU WA DINI. Wote tunaalikwa kumuombea huyu ndugu yetu ambaye alifanya kazi ya Kuwafundisha watu juu ya Mungu na kuwapeleka kwa Mungu kwa mafundisho mbalimbali. APUMZIKE KWA AMANI.