Skip to main content

HABARI ZA JIMBO -Toleo la Januari - Juni, 2015



  1.  SIKU YA MWANAMKE DUNIANI WAWATA WAKUTANA MPANGA
Tarehe 8 Machi ya kila mwaka huadhimishwa kama Siku ya Mwanamke Duniani. Kijimbo, Wanawake wakatoliki maarufu WAWATA waliiadhimisha siku ya Mwanamke Duniani ngazi ya Jimbo katika Tarafa ya Mlimba Parokiani Mpanga. Ilikuwa siku nzuri pale akina mama kutoka parokia mbalimbali walipokutana kwa semina, mafunzo mbalimbali na siku ya kilele Misa Takatifu na michezo. Mgeni rasmi katika kilele hicho alikuwa Mhe. Pd. Bonaventure Mchalange Naibu wa Askofu wa Ifakara. Mahudhurio ya akina mama kadili ya parokia yalikuwa kama inavyoonekana kwenye jedwali.
Na
Parokia
Idadi

Mwendelezo
1
Taweta
16
11
Ifakara
29
2
Mpanga
47
12
Kibaoni
10
3
Mlimba
24
13
Kiberege
2
4
Chita
12
14
Mkula
11
5
Merera
11
15
Msolwa Ujamaa
1
6
Mchombe
21
16
Nyandeo
14
7
Mbingu
26
17
Mofu
0
8
Namwawala
3
18
Lungongole
0
9
Idete
3
19
Kisawasawa
0
10
Mahutanga
2
20
Mang’ula
0
 …….
 ……………………..
……………
21
Kilombero
0
 …….
 ………………………
 …………….
……..
Jumla kuu
232

Katika picha matukio ya siku ya kilele cha siku ya mwanamke kijimbo.
      
    

  1. SR HILTRUDA LYANIHELA ATUTOKA GHAFLA

Ilikuwa taarifa ya ghafla na ya kusikitisha sana pale Mama Mkuu wa Shirika la Masistaa wa Upendo wa Mt. Fransis wa Assis Jimbo la Mahenge alipotutangazia kifo cha Sr. Hiltruda. Sr. Hiltruda alifariki kwa ajali ya kugongwa na pikipiki maarufu “Bodaboda” asubuhi ya jumapili ya tarehe 14 Juni, 2015 eneo la Msimbazi Centre – Dar es Salaam alipokuwa akivuka barabara ya Kawawawa akielekea kanisani kwa misa ya dominika. Msamaria mwema alimwokota Sr. Hiltruda akiwa mahututi na kumkimbiza katika hospitali ya amana – Ilala na baada ya Uongozi wa Shirika kupata taarifa ulikwenda hospitalini na kumhamishia katika hospitali
ya Taifa Muhimbili. Pamoja na juhudi za madtari kuokoa uhai wake, Sr. Hiltruda alifariki dunia majira ya saa 5 asubui. Sr. Hiltruda alizikwa katika makaburi ya Masista Itete tarehe 17 Juni, 2015. Sr. Maria Hiltruda alizaliwa mwaka 1942 Kwiro Mahenge kwa baba Paulo Chigumbi Lyanihela na mama Maria Kamando, amefariki akiwa na umri wa miaka 73. Sr. Hiltruda alitegemewa kuadhimisha jubilei ya miaka 50 ya utawa mwakani, 2016.
APUMZIKE KWA AMANI
 

  1. KWA HERI PADRI DISMAS UBISHIMBALI “STABLE”
 Mtu wa watu, mtani, mcheshi, muwazi, asiye na kinyongo Pd. Dismas Ubishimbali alitoweka ghafla kama utani vile. Ilikuwa asubuhi ya tarehe 30 Mei, 2015 pale Mapadri na Watumishi wa Nyumba ya Mapadri Ifakara walipoingia chumbani mwake alimofikia na kumkuta akiwa amefariki. Pd. Ubishimbali alikuwa amefika Ifakara akitokea Kwiro kwa lengo la kuhudhuria mazishi ya Baba Mdogo wa Padri Filbert Mhasi. Pd. Ubishimbali ambaye alijiita na kutambulika kwa majimba ya utani kama vile “mzungu”, “mzungu mpakistani”, “stable”, nk. Alizaliwa 15/02/1950 kwa baba Clarence Michael Ubishimbali na mama Clara Iddi Antoni Ubaratu. Kwa asili Pd. Ubishimbali ni mzaliwa katika kijiji cha Ebuyu wakati huo ikiwa chini ya Parokia ya Sali Jimbo la Mahenge na familia yake ilihamia Ifakara miaka ya 1964/65. Alisoma Kasita na baadaye Seminari Kuu ya Ntungamo na kumalizia Kipalapala Tabora. Alipata daraja ya ushemasi 29/06/1975 na upadrisho 14/08/1976, madaraja yote aliyapata kwa Askofu Patrick Iteka. Alifariki usiku wa kuamkia 30/05/2015 na kuzikwa Kwiro 02/06/2015. 
APUMZIKE KWA AMANI

  1. SFUCHAS WAOMBOLEZA
Jumuiya ya Chuo Kikuu kishiriki cha Tiba cha Chuo Kikuu cha Mt. Augustino cha Tanzania tawi la Ifakara ilipatwa na msiba mkubwa wa kufiwa na mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho kijana Samweli Lucas. Kijana Samweli alifariki katika ajali ya barabarani katika Mbuga ya Mikumi tarehe 19 Machi, 2015 baada ya basi alilokuwa akisafilia kuja/kurudi Ifakara baada ya likizo fupi ya wiki mbili kugongana uso kwa uso na lori la mizigo na yeye kufariki hapohapo. Marehemu Sanweli alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa kozi ya uganga/udaktari. Kichuo alikuwa Waziri wa Ulinzi katika Serikali ya Wanafunzi ya chuo na mwanamichezo mzuri. Hayati Samweli aliagwa rasmi na jumuiya wa Chuo na wakati wa Ifakara 23/03/2015 na alikizikwa nyumbani kwao Kibaha 24/03/2015. 
APUMZIKE KWA AMANI
                      
Picha ya Marehemu Samweli wakati wa uhai wake           Baba Askofu wa Ifakara na waombolezaji wengine wakitoa heshima zao za mwisho


  1. HOSTELI KIKWAWILA
Mapadri wa Shirika la Utangazaji wa Habari Njema (Heralds of Good News) wanaosimamia kituo cha Watoto Yatima na Wazee cha Kikwawila wamefungua hosteli yao ya wageni iliyokuwa katika ujenzi kwa miaka mingi. Ujenzi wa hosteli hii ulianza na Pd. Fransis aliyekuwa mwanzilishi wa kituo hicho.  Pamoja na nguvu za Shirika, ujenzi wa hosteli hii umepata pia msaada kutoka kwa Wanashirika la “Association Gocce” wa Italia na Mama Maria Tan wa Singapore. Hosteli hii ilibarikiwa na kufunguliwa na Mhashamu Salutaris Libena Askofu wa Ifakara tarehe 16/05/2015 na tukio hilo kushuhudiwa na wawakilishi wa “Association Gocce” ambao ni Anna, Fabian na Torante anayefanyakazi Chuo cha Manesi cha Edgar Maranta.


  1. ASHEREHEKEA MIAKA 20 YA UASKOFU
Mhashamu Agapiti Ndorobo Askofu wa Jimbo la Mahenge aliadhimisha Jubilei Ndogo ya kutimiza Miaka 20 ya Utumishi katika Jimbo la Mahenge kama Askofu. Sherehe hii ilifanyika tarehe 16/06/2015 kwa misa takatifu iliyoanza kuanzia saa 10 jioni katika Kanisa Kuu la Kristo Mfalme Kwiro na baadaye kufuatiwa na tafrija kubwa na nzuri. Askofu Ndorobo alitangazwa kuwa Askofu wa Mahenge 21/03/1995 na kusimikwa rasmi 16/06/1996. Sisi Wanajimbo la Ifakara tunampongeza sana Baba Askofu kwa kutimiza miaka hii ya utumishi kama Askofu na tunamwombea Baraka za Mwenyezi Mungu apate afya njema na nguvu zaidi za kulitumikia taifa la Mungu.



Comments

  1. What is the best gambling site? (2021)
    Casino 군산 출장샵 Sites have the ability to offer some 군포 출장샵 kind of casino services. You can 구리 출장마사지 browse the 태백 출장마사지 list of games and choose 안전 토토 사이트 which ones you want to play.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SHUKRANI YA MAVUNO

Kushukuru ni kuomba, lakini kushukuru ni Uungwana. Mhashamu Baba Askofu Salutaris Libena wa Jimbo Katoliki la Ifakara anayofuraha kubwa sana kuwaalika Mapadre,Watawa na Walei wa Jimbo la Ifakara kwenye adhimisho la Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya Kumshukuru Mungu kwa Neema na Baraka mbalimbali ambazo anatujalia, katika Jimbo letu siku ya Ijumaa ya tarehe 21/09/2012 katika Kanisa Kuu la Jimbo (Ifakara).   Pia katika misa hiyo Askofu, Mapadre, Watawa na Walei wanaungana na Mapadre H. Itatiro, L. Mdenkeri na A. Magome ambao wanatimiza miaka 40 ya Upadre, pia na Padre Kawewela ambaye anatimiza miaka 25 ya Upadre. 

KONGAMANO LA UTOTO MTAKATIFU WA YESU 2013

WATOTO WA UTOTO MTAKATIFU WA YESU Kongamano la Utoto Mtakatifu wa Yesu Kanda ya Mashariki 2013 litafanyika Jimboni Ifakara kuanzia tarehe 13 - 17 ya mwezi wa sita (6). Ni majimbo nane (8) yanayotarajiwa kushiriki katika Kongamano hilo. Majimbo hayo ni:- Dar es Salaam, Morogoro, Mahenge, Tanga, Zanzibar, Dodoma, Kondoa na Ifakara. Maandalizi ya Kongamano hilo yanaendelea vizuri. Mhashamu Askofu Salutaris Libena, Mapadre, Watawa na Waamini wote wa Jimbo la Ifakara wanawakaribisha Watoto wote na watu wote wenye mapenzi mema kufurahia ukarimu wa watu wa Jimbo la Ifakara..                                                     "MTOTO NA IMANI"                               KWA PAMOJA TUNASEMA KARIBUNI SANAA!!  

PADRE LOUIS MDENKERI HATUPO NAE TENA

Padri Louis Adalbert Mdenkeri alikuwa mtoto wa tatu kati ya watoto wanane kwa baba Adalbert Fidelis Mdenkeri na mama Anthonia Kazingoma. Alizaliwa Kwiro tarehe 31 Machi, 1945. Alibatizwa tarehe 01 Aprili, 1945 namba yake ya ubatizo: Kwiro LB 15093. Alipewa kipaimara na Hayati Askofu Mkuu Edgar Maranta tarehe 01 Oktoba, 1955 namba yake ikiwa LN 10026. Alipewa daraja ya Upadri huko Kwiro tarehe 12 Agosti, 1972 na hayati Askofu Adrian Mkoba wa Morogoro.   MAREHEMU PADRE LOUIS  MDENKERI   Elimu: Hayati Padri Mdenkeli alisoma darasa la i-iv katika shule ya Msingi Kwiro. Baadaye seminari ndogo ya Mt. Fransis sasa inafahamika zaidi kama Kasita Seminari darasa la tano hadi la kumi. Baada ya kumaliza darasa la kumi pale Kasita aliacha seminari na kujiunga na sekondari ya Mt. Joseph – Jimbo Kuu la Dar es Salaam ambayo baadaye ikaja kuitwa Forodhani secondary school. Wakati anasoma St. Joseph sekondari, Hayati Sr. Yasinta aliyekuwa Mkuu wa shule alimshauri wakati huo kijana Louis Mk

WATOTO WA KITUO CHA BETHLEHEM WAPATA AJALI

Watoto wapatao 103, Walezi na Wafanyakazi wa Kituo cha Bethlehem jumla yao yapata kama 160 walipata ajali ya gari siku ya jumanne ya tarehe 25 juni, 2013 majira ya saa 11 jioni wakati wakituri kutoka pikiniki. Ajali hiyo ilitokea eneo la Kijiji cha Kilama B baada ya Fuso lililo wabeba kuingia katika shimo na kuanguka. Kati ya Walezi waliopata ajali alikuwepo pia Sr. Salome. Masista wengine walezi walirudi kwa gai nyingine. Mkurugenzi wa Kituo cha Bethlehem, Padri Basil Ngwega alieleza kuwa Watoto, Walezi na Wafanyakazi wa Kituo cha Bethlehem huwa na kawaida ya kufanya pikiniki wakati wanapofunga likizo la mwaka. Na mara hii walichagua kwenda Kilama B kwa pikiniki. Aliendelea kusema kuwa wakati wakirudi, gari ambalo lilibeba kundi kubwa zaidi lilitumbukia kwenye mtaro na kuegama baadaye kuanguka upande wa kulia mwa gari. Katika ajali hiyo, watoto wapatao 20 na walezi 5 waliweza kupata majeraha mbalimbali. Kati yao watoto 2 waliumia kichwani na kushonwa na walezi 4 walipumzishwa kati

KONGAMANO JIMBONI IFAKARA

KONGAMANO LA UTOTO MTAKATIFU KANDA YA MASHARIKI 13 – 17/6/2013 JIMBONI IFAKARA  Jimbo Katoliki Ifakara lilikuwa mwenyeji wa Kongamano la mwaka huu la Utoto Mtakatifu Kanda ya Mashariki ya Metropolitan ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Kongamano hilo lilifanyika kati ya tarehe 13 na 17 Juni, 2013 lilihusisha majimbo manane ambayo ni Ifakara, Mahenge, Morogoro, Dodoma, Kondoa, Tanga, Zanzibar na Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Jumla ya Watoto 2 512 na walezi 570 walishiriki kongamano hili. Jumla hii ya walezi inajumuisha pia Mapadri na Watawa Masista. Maaskofu walioshiriki walikuwa ni pamoja na Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Wahashamu Maaskofu Telesphore Mkude wa Morogoro, Agapit Ndorobo wa Mahenge, Eusebius Nzigirwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Askofu Mwenyeji Salutaris Libena. Jimbo mwenyeji liliwakilishwa na jumla ya watoto 875na walezi 89. Watoto na Walezi kutoka ndani ya Jimbo waliwasili Jimboni tarehe 10 Juni s

TAMASHA LA SHIRIKISHO LA KWAYA ZA KIKRISTO - IFAKARA

Leo tarehe 26/12/2012 Madhehebu ya Kikristo Mjini Ifakara yamefanya Tamasha la Kwaya za Kikristo kama sehemu mojawapo ya Uinjilishaji. Maaskofu wawili walishiriki Tamasha hilo, ambao ni Mhashamu Askofu Salutaris M. Libena wa JImbo Katoliki la Ifakara na Askofu Lenard Mtenji wa KKKT Usharika wa Ifakara. Mhashamu Askofu Salutaris Libena wa Jimbo Katoliki la Ifakara aliwaambia Wanakwaya wa Kwaya zote kuwa Utume wao si kuimba kama wengine wanavyofikiri, bali UTUME WAO NI UINJILISHAJI KWA NJIA YA KUIMBA. Kwa hiyo aliwaambia wanapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwajalia sauti nzuri za kuimba, kwa hiyo wazitumie sauti hizo KUMSIFU, KUMUABUDU, KUMTUKUZA, KUMSHUKURU NA KUMTANGAZA MWENYEZI MUNGU KWA WATU WOTE. Pia aliwaomba watunzi wa nyimbo watunge nyimbo za Kumsifu, Kumtukuza na Kumshukuru Mwenyezi Mungu na Yesu Kristo zaidi kuliko kutunga nyimbo zinazomtaja SHETANI MWANZO MWISHO.Kwani tumepewa silaha za kujikinga na huyo shetani, lakini licha ya kupewa hizo kinga tumepewa sil

KWA HERI KATEKISTA NYONI

Parokia ya Ifakara inasikitika kumpoteza Katekista hodari Pius Pius Nyoni, ambaye Mwenyezi Mungu amependa kumuita kwake. Katekista Nyoni alizaliwa mwaka 1954 huko kijiji cha Sofi. Alipata elimu ya sekondari huko Mahenge Kwiro. Katekista  Nyoni alifanya kazi sehemu mbalimbali kabla ya kuanza kazi ya ukatekista. Alianza kazi ya Ukatekista mwaka 2003 hapa parokiani Ifakara akiwa kama mwezeshaji wa semina mbalimbali hasa katika kundi la wana uamsho. Alipelekwa chuo cha Makatekista na kisha kurudi parokiani na kuwa mwalimu wa dini mzuri. Waliofundishwa naye ndio mashaidi hasa wa utaalamu wa fani yake hii ya mwisho, yaani UALIMU WA DINI. Wote tunaalikwa kumuombea huyu ndugu yetu ambaye alifanya kazi ya Kuwafundisha watu juu ya Mungu na kuwapeleka kwa Mungu kwa mafundisho mbalimbali. APUMZIKE KWA AMANI.

MBIO ZA MWAKA WA IMANI ZA PAMBAMOTO - IFAKARA

MSHUMAA MKUBWA WA MWAKA WA IMANI       Mnamo tarehe ya 17 ya mwezi wa 11 mwaka 2012, Mhashamu Askofu Salutaris M. Libena wa Jimbo Katoliki la Ifakara alizindua rasmi MWAKA WA IMANI katika Kanisa Kuu la Jimbo la Mtakatifu Andrea - Ifakara. Katika Misa hiyo Mhashamu Baba Askofu aliwasha Mshumaa Mkubwa wa Mwaka wa Imani na kisha kuwasha mishumaa midogo kutoka Mshumaa Mkubwa na kuwakabidhi Maparoko kwenda nayo Maparokiani kwo. Na ujumbe "MKAMTANGAZE KRISTO KWA KILA KIUMBE".      Miongoni mwa maazimio ya Mwaka wa Imani Jimboni Ifakara  ni kuutembeza MSALABA katika Parokia zote ndani ya Jimbo. Mbio hizo za kuutembeza Msalaba zimeanza leo tarehe 29/12/2012 kutokea Kanisa kuu la Jimbo na kwenda kukabidhiwa Parokia ya TAWETA ambayo inapakana na Jimbo la Njombe. Msalaba huo umeenda kukabidhiwa na Mhashamu Askofu Salutaris M. Libena.      Ratiba ya mzunguko  wa Msalaba huo imetoka, Safari ya Msalaba itakuwa kama ifuatavyo: Taweta, Mpanga, Mlimba, Chita, Merera, Mchombe, Mbi

TANZIA

TANZIA MAREHEMU SISTA CRESENCIA NGOMBALE TAREHE 14/10/2012 Wahashamu Maaskofu wa Jimbo Katoliki la Ifakara na Mahenge, Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa Upendo wa Mt. Fransisko wa Asizi na Jumuiya ya Mapadri na Watawa wa Majimbo yote mawili wanasikitika kwa Kifo cha Mpendwa wao Sr. Maria Cresencia B. Ngombale. Sr. M. Cresencia Benedict Ngombale ni mzaliwa wa Parokia ya Kipatimu. Alizaliwa Januari 1926 kwa wazazi, Baba:   Benedict Ngombale   Mama: Rozina Namboweto   Jina lake la ubatizo aliitwa Melania Tarehe 09/12/1945 alijiunga rasmi na Shirika la Masista wa Upendo wa Mt. Fransisko wa Asizi – Jimbo la Mahenge kwa kufunga nadhiri za kwanza. Mama Cresencia alikuwa mmojawapo kati ya kundi la pili katika shirika. Katika kipindi cha Unovisi, alisomea ualimu Kwiro – Mahenge, ambayo kwa sasa ni shule ya sekondari ya wasichana ya Mt. Agnes.   Sehemu alizokaa wakati wa uhai wake ni: Kwiro, Ifakara, Sofi, Mofu na Sali kama mwalimu wa shule ya msi