TANZIA
MAREHEMU SISTA
CRESENCIA NGOMBALE
TAREHE
14/10/2012
Wahashamu
Maaskofu wa Jimbo Katoliki la Ifakara na Mahenge, Mama Mkuu wa Shirika la
Masista wa Upendo wa Mt. Fransisko wa Asizi na Jumuiya ya Mapadri na Watawa wa
Majimbo yote mawili wanasikitika kwa Kifo cha Mpendwa wao Sr. Maria Cresencia
B. Ngombale.
- Sr. M. Cresencia Benedict Ngombale ni mzaliwa wa Parokia ya Kipatimu.
- Alizaliwa Januari 1926 kwa wazazi,
- Baba: Benedict Ngombale
- Mama: Rozina Namboweto
- Jina lake la ubatizo aliitwa Melania
- Tarehe 09/12/1945 alijiunga rasmi na Shirika la Masista wa Upendo wa Mt. Fransisko wa Asizi – Jimbo la Mahenge kwa kufunga nadhiri za kwanza.
- Mama Cresencia alikuwa mmojawapo kati ya kundi la pili katika shirika.
- Katika kipindi cha Unovisi, alisomea ualimu Kwiro – Mahenge, ambayo kwa sasa ni shule ya sekondari ya wasichana ya Mt. Agnes.
- Sehemu alizokaa wakati wa uhai wake ni: Kwiro, Ifakara, Sofi, Mofu na Sali kama mwalimu wa shule ya msingi. Mpanga kama mkatekista na Betlehemu kama mama mkubwa. Aliwahi pia kulea Wanovisi wetu kule Itete.
- Mwaka 1996 alihamia Mbingu alikaa huko mpaka kifo chake.
- Sr. Cresencia alikuwa na umri wa miaka 86.
- Mungu ampumzishe kwa amani. AMINA
Comments
Post a Comment